Fahamu zaidi kuhusu maisha, Imani na Mungu

Mafunzo ya Alpha ni kozi ya wiki kadhaa inayokupa fursa.

<< Back to English

Alpha ni Nini?

Alpha ni mfululizo wa vipindi vinavyoangazia Imani ya Kikristo. Kila mada inatazama swali tofauti kuhusu imani na imebuniwa kuibua mazungumzo. Mafunzo ya Alpha yanaendeshwa kote duniani na kila mmoja anakaribiswa. Yanaendeshwa mtandaoni, kwenye mikahawa, makanisani, vyuo vikuu, majumbani-kila mahali! Mikutano ya Alpha hainafanani, lakini kwa ujumla wake ina mambo muhimu matatu ya msingi: ukarimu, mada na mazungumzo mazuri.

Alpha in Swahili

Kipindi cha Alpha kinakuwaje?

Unganishwa

Iwe wakati wa chakula au mmekutana mtandaoni mkinywa chai, vipindi vyote huanza na wakati wa kufahamiana, kupumzika na kujenga mahusiano. Kula chakula pamoja kunatengeneza nafasi ya watu kufahamiana na kushirikishana maisha kwa kina zaidi.

Find-an-alpha

Tazama

Mada za Alpha zimeundwa kuwahusisha watu wa viwango vyote vya maisha na kuchochea mazungumzo. Zinagusa kwa kina masuala makubwa ya maisha na kufungua misingi ya Imani ya Kikristo, zikijibu maswali kama, ‘Yesu ni nani?’ au ‘Mungu anatuongoza vipi?’

Jadili

Muda wa majadiliano ni fursa kwa watu kuitikia mada, kusikia kutoka kwa wengine na kuchangia mtazamo wao kwa nia ya dhati, kirafiki na katika mazingira ya uwazi.

Mapitio ya Maudhui ya Mada za Alpha

Anza Mafunzo

Tumetengeneza kila unachohitaji kukusaidia katika kila hatua unayochukua. 

MyAlpha (AlphaYangu) ni jukwaa la mtandaoni na chanzo kizuri cha bure cha kushirikisha Alpha. Humo utakuta zana zote/ vyote unavyohitaji, Msaada na kila unachohitaji kuendesha Alpha ikiwemo Mada za Alpha, Mafunzo ya Alpha, Nyenzo za kutangaza Alpha na mfululizo wa mafunzo yake.

Anza Kuomba

Moja ya vipengele vya kipekee kabisa vya Alpha ni udhabiti wake wenye msisitizo katika maombi. Uwe na timu ya maombi inayoombea wageni kila siku wakati wa kipindi chote cha Alpha. Kama hatutamtanguliza Mungu, juhudi zetu hazitazaa matunda. Huu ni mtembeo wa Roho Mtakatifu ambao sisi ni sehemu yake.

Ipe Timu Mafunzo

Ukiipata timu yako tayari, haraka ni wakati wa kuwapa ujuzi wa namna ya kuendesha Alpha. Wanaweza kuhudhuria mafunzo kwa njia ya mtandao au ana kwa ana, au unaweza kutumia video ya mafunzo kwa timu, ni nyenzo nzuri sana ya wenyeji wa kundi na wasaidizi kwa timu yako.

Tangaza Kanisani kwako

Alpha imetengeneza nyenzo nzuri za matangazo kukusaidia kueneza Neno. Kuwafanya wengine kanisani kwako kujua kuhusu Alpha ni njia kuu ya kusaidia kumpa fursa kila mmoja kuwakaribisha wengine washiriki kufahamu zaidi Imani. Jaribu kuwashirikisha simulizi kabla ya kuanza Alpha.

Karibisha Wageni

Wakati unaifunza timu yako, watie moyo kuendelea kuombea na kuwakaribisha wengine kuja Alpha. Mwaliko wa dhati kushiriki Alpha ndio kitu bora zaidi. Tumefanya iwe rahisi kwa nyenzo zilizopo kwenye MyAlpha(AlphaYangu) kutumia ‘kama ilivyo’ au kuifanya rafiki kwako.

Ridhaa za Alpha Swahili

Bishop Calisto
AYS Ep1 Preview
Bishop Edith
Bishop Kepha
Ps Anthony
Rev Kwame
previous arrow
next arrow

Injili ni bure – Vivyo hivyo Alpha

questions

Uko tayari Kuendesha Alpha?

Skip to content